MENTORSHIP PROGRAM

Mentorship program ni program inayotolewa na AMKA MTANZANIA ambapo kupitia program hii mshiriki anaweza kujifunza na kuongeza ujuzi wake katika Nyanja zifuatazo;
1. Kuanzisha na kukuza biashara.
2. Uandishi wa makala na vitabu.
3. Uanzishaji uendeshaji na ukuzaji wa blog.
4. Biashara ya kwenye mtandao na kutengeneza pesa kwenye intanet.
5. Kujifunza mbinu za kuboresha na kuongeza thamani kwenye kazi yako.
6. Kujijengea tabia ya kupenda kujisomea.
7. Kubadili tabia zinazokurudisha nyuma kama ulevi, uvivu, kukata tama.
8. Kujenga tabia ya kuweka akiba na kuwa na matumizi mazuri ya fedha.
9. Kujenga tabia ya kuwa na matumizi mazuri ya muda.
10.Kujifunza mambo mapya ili kuongeza ujuzi na utaalamu.

Muundo wa kuendesha program.
Program hii itaendeshwa kulingana na mahitaji ya mlengwa. Mtu atakapojiunga na program hii atajadiliana na MENTOR kisha wataweka malengo pamoja na kukubaliana majukumu ambayo mtu atatekeleza kila siku na kila wiki. Baada ya hapo MENTOR atakuwa anafuatilia kwa karibu utekelezaji wa majukumu na makubaliano.
Ufatiliaji unaweza kuwa kila siku au kila wiki kulingana na uchaguzi wa mhusika. Yote haya yatafanyika kwa njia ya mtandao na mawasiliano kwa simu.
Lengo kubwa la program hii ni kumjengea mshiriki nidhamu ya kuweza kupanga na kufuata mipango yake mwenyewe. Kila mtu anaweza kujifunza mambo mapya na mazuri ila kinachokosekana ni nidhamu ya kufanya hivyo. Kupitia program hii utasimamiwa ili kujenga nidhamu ya kuweza kufanya kile ulichopanga kufanya.
Kufanikiwa kwa program hii kutategemea juhudi za mhusika mwenyewe. Kwa yeyote mwenye juhudi atafanikiwa kwa kiwango kikubwa. Kwa asiyekuwa na juhudi atashindwa kufanikiwa.
Gharama za program.
Gharama za program zitategemea sana ukaribu na idadi ya siku ambazo mshiriki atawasiliana na MENTOR katika ufuatiliaji.
1. Kwa atakayependelea kufuatiliwa kila siku atalipa gharama ya tsh 300,000/= kwa mwezi.
2. Kwa atakayependa kufuatiliwa siku tatu kwa wiki atalipa tsh 200,000/= kwa mwezi.
3. Kwa atakayependelea kufuatiliwa siku moja kwa wiki atalipa tsh 100,000/= kwa mwezi.
Malipo yanafanyika kabla ya program kuanza au kuendelea.
Kwa mtu ambaye ana kiu kubwa ya kujifunza mwezi mmoja au miwili inamtosha kujifunza kitu chochote kile anachopenda kujifunza.
Karibu sana kwenye program hii.
Mawasiliano;
Makirita Amani,
0717396253/0755953887