Karibu AMKA CONSULTANTS

AMKA CONSULTANTS ni kampuni inayojihusisha na kutoa ushauri, mafunzo na uhamasishaji wa watu kuweza kufikia uzalishaji mkubwa kwenye kazi au biashara zao na kuweza kufikia mafanikio makubwa. Kupitia AMKA CONSULTANTS utaweza kupata mafunzo mbalimbali kwa njia ya mtandao, semina na ushauri wa ana kwa ana. Mafunzo haya yatakuwezesha wewe kutumiwa uwezo mkubwa ambao tayari upo ndani yako. Kila binadamu anao uwezo mkubwa sana, ila watu wengi wanakosa maarifa na hamasa ya kutumia uwezo wao. Kupitia AMKA CONSULTANTS utapata MAARIFA na HAMASA ya kuweza kufikia mafanikio makubwa zaidi kwenye maisha yako bila ya kujali UMRI WAKO, KABILA LAKO, RANGI YAKO au ELIMU YAKO. Hakuna kinachokuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa ila wewe mwenyewe. Sababu zote unazofikiria sio za kweli na kupitia AMKA CONSULTANTS utajifunza jinsi ya kuondokana na sababu hizo za uongo zinazokurudisha nyuma. Kujua zaidi kuhusu huduma zetu bonyeza HUDUMA ZETU.